Hapa nilikuwa namwelekeza kitu wakati wa upigaji picha ya Family Tears 2008
“Hakuna
kitu kizuri duniani kama kuifanya dunia hii kuwa darasa kwako, jifunze kwa kila
mtu, hata kichaa aweza kuwa mwalimu kwako, kama hutajifunza chochote toka kwa
kichaa basi hata kutoautisha tu mwenye akili kwa kumlinganisha na huyo kichaa
ni darasa tosha…”
Nakumbuka maneno haya nilimwandikia Hayati Steven Charles
Kusekwa Kanumba katika moja ya script chakwa zilizomkuza na ikawa ni dira
katika maisha yake. Nitaikosa sana tabia yake hii ya kuwa msikilizaji kuliko
mbishani, alipenda sana kujifunza na kudadisi mno kwa kitu ambacho hakukijua,
hakuwa mjuvi kwa jambo asilojua, na akilijua basi hulizingatia, Tunapaswa kuiga
tabia hii kama kweli tunataka kubakisha historia nyuma yetu.
bro kiukweli nafurahia kuifanya dunia kuwa darasa kwangu, wewe umekuwa mwalimu kwangu pale ninapotamani kufanya kazi nzuri kama za kwako(uandishi bora wa script) na pia brother jb anazidi kuwa mwalimu kwangu pale ninapofikiria kuwa actor mkubwa kama yeye hvyo naifurahia dunia kuwa darasa huru kwangu nisilochangia hata shilingi kumi, Marehemu steven kanumba tutamkumbuka daima kwa kuipeleka sanaa yetu mbali na kututambulisha kimataifa kama isingekuwa mauti angeipeleka sanaa yetu hadi hollywood, ila kazi ya mungu haina makosa tumwombee alale salama katika makazi yake ya kudumu, naitwa Mussa mwakitinya
ReplyDelete