Mimi na hayati Steven Kanumba baada ya kuchukua tuzo zetu mwaka 2010
Kuna tatizo hili Tanzania, sijui niseme ni sugu
au niliiteje? Hakuna chombo au taasisi maalumu inayohusika moja kwa moja na
utoaji wa Tuzo za Filamu....Sijajua sababu hasa ni nini. Mwaka 1999, kulikuwa
na Tuzo zilizojumuisha kada mbali mbali filamu ikiwa mojawapo, na ninakumbuka
aliyeibuka kuwa msanii bora wa kiume alikuwa Richie Richie, wengine siwakumbuki
pengine kwa sababu hawapo tena kwenye tasnia, tuzo hizo ziliandaliwa na M-net.
Mwaka 2006 (Kama sikosei), kul,ikuwa na Tuzo za Risasi zilizoandaliwa na Gazeti
lka Risasi, na msanii bora wa kiume alikuwa Dimoso, wakati msanii bora wa kike
alikuwa Riyama. Mwaka 2008 kulikuwa na Vinara Awards ambapo Msanii bora wa
kiume alikuwa Jacob Steven na Msanii bora wa Kike alikuwa (Simkumbuki jina) ila
Irene Uwoya na Yusuf Mlela walipata tuzo ya up coming wakati Steven Kanumba
akiambulkia tuzo ya heshima. Mwaka 2010 kulikuwa na tuzo za Filamu Central,
ambapo Mimi nilishinda nafasi ya mwandishi bora wa Mwaka, Steven Kanumba
alishinda Mugizaji bora wa Mwaka, Monalisa lishinda muigizaji bora wa kike wa
mwaka, Vincent Kigosi alishinda tuzo ya muongozaji bora wa mwaka na
mtayarishaji bora wa mwaka. Kukafuatia tuzo ambazo hazina utaratibu na hata
zote ambazo nimekuwa nikizitaja huwa zinafanya mara moja halafu hazirudii tena,
labda ZIFF kidogo naona wana utaratibu wa kuwa na tuzo kila mwaka, sijui sasa
watu huandaa wakiwa wanatarajia kitu tofauti na uhalisia? Hebu tuchangieni
unapoweka tuzo ambazo ni za kudumu zinaleta hamasa sana katika tasnia, mfano mzuri ni tuzo za kilimanjaro tanzania music award ni tuzo ambazo hutolewa na mdau mmoja ambaye ni bia ya kilimanjaro na zina hamasa kubwa katika tasnia ya filamu,hvyo imefika muda wa wadau wa tasnia ya filamu(cosota,makampuni na wizara husika) kuungana na kuanzisha tunzo ambazo zitadumu npaka milele kwani tukifanya hivyo tutakuwa tunaleta hamasa kubwa katika tasnia ya filamu, mimi yangu ni hayo tu!
ReplyDeletekilimanjaro tanzania music award nikimaanisha tunzo zenye amasa katika tasnia ya mziki hvyo wadau wa filamu lazima waangalie hili swala kiundani
ReplyDeleteHapo Kaka kwa mm nawezasema walikuwa waanfanya hivyo kwa manufaa yao na baaada ya kupata kile walichokitalajia wanachana na hilo swala mbona Kili ni za kila mwaka au hiz za Zanzibar Festival...! Zinakuwaa kila mwaka au zinaajirudia lakin nying hapo umezitajaa ni kweli sijazisikia tena tangu hapo, kwaahiyo nawezasema wanakuwa wanatafuta wanachokiaonaa kwao kinawanufaisha tu.
ReplyDelete