CHAMA cha Waigizaji Mkoa wa Kinondoni kinazinduliwa rasmi siku ya jumatatu tarehe 12/ 9/ 2011 katika ukumbi wa Vijana Kinondoni, mkutano huu unawakutanisha wasanii wote wa eneo hili la Kinondoni kwa ajili ya usajili wa wasanii na kuutambulisha uongozi uliopo madarakani , siku hii pia itatumika katika kupanga mikakati katika kujiletea maendeleo. Katika mkutano huu mgeni wa heshima ni Naibu Waziri Wa Habari Vijana, Utamaduni Na Michezo Dk.Fenela Mukangara , pia siku hii utaendeshwa harambee kwa ajili ya kuchangia chama, kwa matumizi ya Chama hicho. Akiongea na FC Mwenyekiti wa Chama hiki Adam Melele (Swebe) amesisitiza wasanii kujitokeza kwa wingi kwani tayari mikakati ya kimaendeleo ndiyo hasa lengo la uanzishaji wa vyama ambavyo kwa sasa vipo katika michakato ya kuwaunganisha wasanii kwa kuwaongoza.
"Tukiwa pamoja ni rahisi sana kujua matatizo yetu na njia sahihi katika kuyatatua, lakini bila umoja hakuna jambo litakalofanyika katika kuijenga sanaa hii, ambayo ni imani yetu kuwa endapo itatumiwa vema ni ukombozi kwa vijana” Swebe.
Mkutano utaanza saa nne kamili asubuhi katika ukumbi wa Vijana maeneo ya Kinondoni jirani na Mango Garden.