Saturday, September 10, 2011

MTANZANIA ANAYETESA HOLLYWOOD HUYU HAPA.

                                                 Rachel Zawadi Ruttrell

Alizaliwa tarehe 19 januari mwaka 1971 Lushoto Tanga kwa baba Mmarekani kutoka Louisiana na mama Mtanzania. Familia yake ilihamia nchini Canada mwaka 1976, wakati yeye ana miaka mitano ambako ameendelea kuishi mpaka leo hii. Baba yake alikuwa mwanachama wa kikundi cha Toronto Mendelssohn choir, ambapo pia alimfundisha Rachel sauti ya soprano. Rachel pia alijifunza kucheza muziki aina ya ballet katika shule Russian Academy of Classical Ballet School, pia alijifunza kupiga piano katika shule ya Royal Conservatory of Music ya Toronto. Mafunzo ya muziki yalimvuta Rachel katika kuigiza, ambapo alianza kuigiza katika tamthiliya kama Miss Saigon, na baadae Goblin market na Once on this Island. Pia amepata sifa kubwa sana katika tamthiliya ya Stargate Atlantis...Kitu kikubwa kwake, anajivunia kuzaliwa Tanzania.

2 comments:

  1. Karibuni wadau, nangojea michango yenu.

    ReplyDelete
  2. Tanzania ina zidi kufungukiwa milango yake huko kwenye mataifa yaliyo komaa kwenye tasnia ya filamu...much love kwa Zawadi.

    ReplyDelete