Saturday, September 10, 2011

Naweza kusema watu hawa ndicho kioo changu

                                        Tyler Perry
       Mwandishi wa Filamu, michezo ya jukwaani na mwigizaji mahiri.



                                           Sidney Sheldon
                              Mwandishi mahiri wa Riwaya

Nakumbuka kuna mwalimu wangu mmoja aliwahi kuniambia kuwa, kama unataka kuwa mahiri katika jambo lolote lile, lazima uwe na mtu wa kumuiga (role model), na tangu nilipoambiwa hivyo, nimekuwa nikijaribu kujitafuta hasa mtindo ninaupenda sana huwa ninaupata wapi, nimejikuta nikigundua watu hawa wawili; mmoja akiwa mwandishi mahiri wa riwaya (novel); kitu ambacho nami pia nakifanya, mtu ambaye kabla hajaanza kuandika novel, alikuwa mwandishi wa filamu kwa miaka kumi na saba Hollywood na kupata tuzo kadhaa, mtu huyo ni Sidney Sheldon. Na mwingine akiwa ni mwandishi mahiri wa miswada ya filamu (script), pamoja na michezo ya jukwaani, ikiwa ni pamoja na kuigiza nafasi nyingi na kuzimudu vema. Mtu huyo ni Tyler Perry. watu hawa naweza kusema ni kioo changu katika sanaa.

1 comment:

  1. bila ya kuwa na role model katika kazi unazofanya bado haujawa na malengo ya kufika katika kilele cha mafanikio, naitwa mussa mwakitinya

    ReplyDelete